59. PELELEZA NDANI YANGU

PELELEZA NDANI YANGU
 
1.  Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako 
Mungu,
Idhihiri pia.
 
2.  Peleleza moyo wangu
Unifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.
 
3.  Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.
 
4.  Peleleza na mawazo
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo – umbo.
 
5.  Zidi kuyapeleleza
Katikati yangu
Hata wishe nifundisha
Udhaifu wangu.
 
6.  Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U Mpenzi wangu.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA