44. KUKAWA NA GIZA DUNIA YOTE

KUKAWA NA GIZA DUNIA YOTE

1.  Kukawa na giza dunia yote,
Ni Mwanga wa ulimwengu,
Ikaisha ulipokuja yote,
Ni mwanga wa ulimwengu.
 
Chorus:
Jua, Yesu hana mwenziwe!
Nalipofuka kama wewe;
Nakwombea umwone nawe,
Ni mwanga wa ulimwengu.
 
2.  Hatuna giza tudumuo mwake,
Ni mwanga wa ulimwengu;
Tumwandamiapo nyayoni mwake
Ni mwanga wa ulimwengu.
 
3.  Enyi wa gizani wenye kutanga!
Ni Mwanga wa ulimwengu,
Kaulekeeni, mpate lenga;
Ni mwanga wa ulimwengu.
 
4.  Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu
Ni Mwanga wa ulimwengu;
Ni nuru za mbingu Kondoo wa Mungu
Ni mwanga wa ulimwengu.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA