46. TWAE WANGU UZIMA

TWAE WANGU UZIMA

1.  Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku
Zikutukuze huku.
 
2.  Twae mikono nayo,
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.
 
3.  Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.
 
4.  Twae dhambi pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.
 
5.  Njia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.
 
6.  Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA