47. NI WAKO WEWE

NI WAKO WEWE

1.  Ni wako wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako, 
Nizidi kusongea.

Chorus:
Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Sana, kwako mtini.
Bwana vuta, vuta nije, nisongee,
Pa damu ya thamani.
 
2.  Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;\
Uyapendayo nami nipende,
Nizidi kukwandama.
 
3.  Nina furaha tele kila saa
Nizungumzayo kwako,
Nikuombapo nami napata 
Kujua nia yako.
 
4.  Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng’ambo ya liko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA