48. NAWEKA DHAMBI ZANGU

NAWEKA DHAMBI ZANGU

1.  Naweka dhambi zangu
Juu yake Bwana
Kuziondoa, kwangu
Hulemea sana;
Na uaili wangu
Ameuondoa;
Dawa yangu ni damu,
Kwa hiyo napoa.
 
2.  Na uhitaji wangu
Nitamjuvisha,
Kwa upungufu wangu
Yeye anatosha;
Majonzi yangu yote
Na mizigo yangu,
Atachukua vyote
Yesu Bwana wangu.
 
3.  Na roho yangu nayo,
Imechoka sana;
Namletea hiyo
Ilindwe na Bwana;
Ni jema jina lake,
Nalo lapendeza,
Imanweli na kwake
Tutalitukuza.
 
4.  Natamani daima
Niwe kama Bwana,
Mpole, tena mwema,
Wa mapenzi sana;
Zaidi natamani
Kwenda kwake juu,
Nikaone mbinguni
Enzi yake kuu.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA