50. YESU NAKUPENDA, U MALI YANGU

YESU NAKUPENDA, U MALI YANGU

1.  Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
2.  Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
3.  Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
4.  Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
 
5.  Mawanda mazuri, na maskani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA