KIVULINI MWA YESU 1. Kivulini mwa Yesu kuna Kituo: Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu. Chorus: Kivulini mwa Yesu kuna kituo; Kivulini mwa Yesu kuna kituo; Raha tu, mle; amani tupu. Furaha tele; kivulini mwa Yesu Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu. 2. Kivulini mwa Yesu nina amani Iliyopita fahamu, tena itakayodumu. 3. Kivulini mwa Yesu nina furaha; Furaha yenye fahari, ya kueneza habari.
PELELEZA NDANI YANGU 1. Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia. 2. Peleleza moyo wangu Unifunulie, Yaliyomo ndani yangu Nami niyajue. 3. Kwanza washe zako tambi, Kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza. 4. Peleleza na mawazo Ni mbegu za mambo, Asili ya machukizo, Maumbuo – umbo. 5. Zidi kuyapeleleza Katikati yangu Hata wishe nifundisha Udhaifu wangu. 6. Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu, Hakika nitakujua U Mpenzi wangu.
WAITWA, MWOVU NA BWANA 1. W aitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako? Chorus: Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni. 2. Alilipa damu yake Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema. 3. Ukifanywa kuwa mwema Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani. 4. Ni mwanga tu, nchi ile, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke.
Comments
Post a Comment