54. YESU NATAKA KUTAKASWA SANA

YESU NATAKA KUTAKASWA SANA

1.  Yesu nataka kutakaswa sana,
Nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka
Unioshe sasa niwe mweupe.

Chorus: 
Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.
 
2.  Bwaba Yesu, unitazame sasa,
Unifanye niwe dhabihu hai;
Najitoa kwako, na moyo wote;
Unioshe sasa niwe mweupe.
 
3.  Bwana kwa hiyo nakuomba sana,
Nakungojea miguuni pako,
Naomba unioshe damuni tu,
Unioshe sasa niwe mweupe.
 
4.  Bwana ninadumu kukungojea,
Niumbie moyo safi, Ee Mungu,
Wanaokujia hutupi kamwe,
Unioshe sasa niwe mweupe.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA