55. NIPE MOYO WENYE SIFA

NIPE MOYO WENYE SIFA

1.  Nipe moyo wenye sifa
Sio wa utumwa;
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani.
 
2.  Moyo maskini, moyo
Wa kunyenyekea,
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia.
 
3.  Mwenye kutubu, mnyonge,
Sadiki, amini;
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani.
 
4.  Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi.
 
5.  Ni uule moyo wako;
Moyo wa huruma
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema.
 
6.  Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami;
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi.
 
7.  Nitie yako tabia,
Inishukie juu;
Jina lako nipe pia,
Ndilo la pendo tu.
 
8.  Ni wa Baba utukufu;
Mwana atukuke;
Na roho Mtakatifu
U Utatu pweke.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA