56. NI SIKU KUU SIKU ILE

NI SIKU KUU SIKU ILE

1.  Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
Kunyamaza hauwezi.

Chorus:
Siku kuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa dambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Siku kuu! siku kuu!
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
 
2.  Tumekwisha kupatana
Mimi wake, Yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
Nikiri neno la Mungu.
 
3.  Moyo tulia kwa Bwana
Kiini cha raha yako,
Huna njia mbili tena;
Yesu ndiye njia yako.
 
4.  Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima,
Hata ije siku ile,
Ya kwonana kwa salama.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA