58. MWAMBA WENYE IMARA

MWAMBA WENYE IMARA

1.  Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.
 
2.  Kwa kazi zote pia ,
Sitimizi sharia.
Nijapofanya bidii,
Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.
 
3.  Sina cha mkononi,
Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.
 
4.  Nikungojapo chini,
Nakwenda kaburini;
Nipaapo Mbinguni,
Na kukwona enzini:
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA