60. WAPONYENI WATU WAMO KIFONI

WAPONYENI WATU WAMO KIFONI

1.  Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni walio shimoni;
Na aangukaye mumzuie;
Ya Bwana Yesu wahubirini.

Chorus: 
Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko, wahubirini.
 
2.  Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Msiwadharau, muwaonyeni;
Huwasamehe; wakiamini.
 
3.  Myoyoni mwa ndani, yule shetani
Ameyaseta mawazo yao;
Lakini kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta kwa pole hao.
 
4.  Kawaokoeni, waje njiani,
Mutimize mapenzi ya Bwana;
Na kwa nguvu zake warudi kwake,
Kwa subira waonyeni sana.

Comments

Popular posts from this blog

42. KIVULINI MWA YESU

59. PELELEZA NDANI YANGU

37. WAITWA, MWOVU NA BWANA